Rais Magufuli aongoza kikao cha kamati kuu ya CCM

0
130

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kikao hicho cha Kamati Kuu kinachofanyika leo kitafuatiwa na kingine cha Halmashauri Kuu ya Taifa kesho Jumanne.

Taarifa iliyotolewa awali na Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey Polepole imesema vikao hivyo pamoja na mambo mengine vitakuwa na ajenda ya kupokea tathmini ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 ambao kampeni zake zinaendelea.

Polepole amesema kuwa “Ajenda nyingine ya vikao hivi vya uongozi vya kitaifa itakuwa kupokea, kuchuja, kutoa mapendekezo na kufanya uteuzi wa mwisho katika ngazi ya mikoa na taifa katika chama na jumuiya zake kwa maana ya umoja wa vijana, wanawake na wazazi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017.

LEAVE A REPLY