Rais Magufuli amuapisha balozi wa Tanzania nchini Malawi

0
188

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mhe. Benedict Martin Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi

Mhe Benedict Martin Mashiba amechukua nafasi ya Mhe. Victoria Richard Mwakasege ambaye amestaafu nafasi hiyo, mbali na hilo Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho wa Mabalozi watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mbali na hilo Rais Magufuli amewapongeza mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na kuwaomba mabalozi hao kutilia mkazo diplomasia ya Uchumi kwa kuongeza juhudi za kuhamasisha wafanyabiashara na wadau wengine wa maendeleo kushirikiana na Tanzania katika biashara na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo ujenzi wa viwanda, Kilimo na huduma za jamii.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni

1.Mhe. Nguyen Kim Doahn – Balozi wa Vietnam hapa nchini.

2.Mhe. Prof. Ratlan Pardede – Balozi wa Indonesia hapa nchini.

3.Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solcynski–Balozi wa Vatican hapa nchini.

4.Mhe. Dkt. Detlef Wachter – Balozi wa Ujerumani hapa nchini.

5.Mhe. Richard Tumisiime Kabonero – Balozi wa Uganda hapa nchini

LEAVE A REPLY