Rais Magufuli ammwagisa sifa Mizengo Pinda

0
173

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza  Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda kwa kumwelezea ni kiongozi mkimya na asiyependa kuzungumza ovyo ovyo.

Rais Magufuli amesema Pinda, maarufu kama Mtoto wa Mkulima, ni kiongozi anayefaa kuigwa na viongozi wengine, na kwamba hata yeye siku akistaafu atamfuata ili kujifunza.

Aliyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akifungua Tawi la Benki ya NMB la Kambarage na Jengo la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Sifa kwa Pinda zinakuja miezi saba tangu alipokosoa viongozi wastaafu wa “maeneo mengine” wanaosemasema kila wakati kuhusu uendeshaji wa serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Septemba 11, mwaka jana Rais Magufuli alitoa mfano wa majaji wastaafu ambao alisema ni tofauti na wastaafu wengine na kwamba huenda kujua sheria ndiko kunakowasaidia kutokuwa waropokaji.

LEAVE A REPLY