Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi kuongeza nguvu kupambana na dawa za kulevya

0
144

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa kumuapisha kamishna mkuu wa mamlaka ya kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya, Rogers William Sianga Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amewataka viongozi wote wa Serikali kuungana na vyombo vya dola kwenye mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya hapa nchini.

Rais Magufuli amewapongeza viongozi wa mikoa walioanzisha vita hiyo ya madawa ya kulevya akiwemo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Pia Rais Magufuli amewataka wananchi kuunga mkono jitihada za kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya hapa nchini.

LEAVE A REPLY