Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Bandarini jijini Dar es Salaam

0
273

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzAnia, Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza bandari kuu jijini Dar es salaam.

 

Rais Magufuli amekagua matanki ya mafuta ya kula ambayo yameadimika hapa nchini na kubaini udanganyifu mkubwa wenye lengo la kukwepa kodi.

 

Rais Magufuli amewataka wamiliki wa mafuta hayo kulipa ushuru wake unaostahili pamoja na faini kutokana na udanganyifu huo ulioufanyika.

 

Pia Rais Magufuli amemtaka mkemia Mkuu wa Serikali kufuata maadili ya kazi, ili kuleta weledi na kujenga nchi.

 

Amesema kuwa “Mkemia Mkuu nataka sampo zozote mtakazokuwa mnapewa fanyeni kwa utaratibu kwa kuzingatia maadili, mkiletewa mkono wa albino semeni mkono wa albino msije mkasema mkono wa mbwa. Mkiletewa madawa ya kulevya semeni haya ni madawa ya kulevya sio unga wa muhogo.

LEAVE A REPLY