Rais Kenyatta asaini sheria za uhalifu wa mtandao

0
137

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameidhinisha mswada wa sheria za uhalifu wa mtandaoni wa 2018 kuwa sheria.

Sheria hiyo itatoa adhabu ya faini ya dola 50,000/=, kifungo cha miaka miwili jela au adhabu zote mbili kwa atakayetoa habari feki au mtu yeyote atakayebainika kuwa na makosa ya mtandaoni.

Kadharika kwa mtu atakaye toa taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu sheria hiyo inasema atafungwa jela zaidi ya miaka kumi.

Hatua hiyo imepokelewa kwa hisia na maoni tofauti kwa watu mbalimbali ambapo kiongozi wa zamani wa chama cha wanasheria Kenya Apollo Mboya amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kifungu hicho kinaweza kuwapa watawala ‘uhuru’ wa kukandamiza vyombo vya habari.

Kwa upande mwingine shirika la kimataifa la kutetea uhuru wa wanahabari Committee to Protect Journalists (CPJ) nalo limekuwa likipinga uidhinishaji wa mswada huo.

LEAVE A REPLY