Rais Al-Bashir aagiza kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa nchini Sudan

0
198

Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir ameagiza kuachiwa kwa wafungwa wote wa kisiasa wanaoshikiliwa kwenye magereza nchini humo.

 

Uamuzi huo umekuja wakati ambapo vyama vya siasa na makundi ya asasi za kiraia nchini humo vimeshiriki mijadala ya kitaifa inayoendelea ikihusisha wawakilishi wa Serikali.

 

Bashir ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 1989 amesema kuwa hatagombea tena urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.

 

Tangu mwaka 2015, Serikali ya Bashir imekuwa ikifanya mikutano na viongozi wa upinzani pamoja na makundi ya waasi kupitia mijadala ya kitaifa.

 

Hiyo ni sehemu ya juhudi za kumaliza migogoro inayoendelea katika maeneo yenye vita kama Darfur.

LEAVE A REPLY