Raia watatu wa Nigeria wanyongwa Indonesia kwa dawa za kulevya

0
140

Serikali ya Indonesia imetekeleza adhabu ya kifo kwa kwa wafungwa wanne wa dawa za kulevya ikiwemo wafungwa watatu kutoka nchini Nigeria.

Watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi muda mfupi baada ya kutimu saa sita usiku za nchi hiyo sawa na saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye jela ya Nusakambangan.

Wafungwa wengine 10 waliohukumiwa adhabu hiyo na mbao walitarajia kukumbwa na adhabu hiyo jana walipata ruhusa ya dakika ya mwisho ya kuendelea kusubiri.

Shirika la Amnesty International limelaani utekelezaji wa adhabu hiyo na kuiita ‘kitendo kisichokubalika kabisa’ kinachokiuka sheria za ndani na kimataifa.

Naibu mwanasheria mkuu wa Indonesia, Noor Rachmad amesema kuwa ‘sio kitendo cha kufurahisha lakini ni utekelezaji wa sheria’.

‘Unyongaji unalenga kukomesha makosa ya dawa za kulevya’

Indonesia inasifika kwa kuwa na sheria kali za dawa za kulevya na imekuwa ikikumbana na malalamiko mengi kimataifa baada ya kurudisha adhabu ya kunyonga.

Mwaka 2015, wafungwa 14 wa dawa za kulevya wengi wao wakiwa wageni walinyongwa mwezi Aprili na kuibua malalamiko makubwa kutoka kwenye taasisi za kutetea haki za binadamu duniani.

Wafungwa walionyongwa jana wametajwa kuwa ni raia wa Indonesia Freddy Budiman na raia wa Nigeria Seck Osmane, Humphrey Jefferson Ejike na Michael Titus Igweh.

LEAVE A REPLY