Raia wa Zimbabwe nchini Uingereza washangilia Mugabe kutolewa madarakani

0
178

Raia wa Zimbabwe wanaoishi uhamishoni London walikusanyika nje ya ubalozi wa taifa hilo nchini Uingereza, kusherehekea kinachoonekana kuwa kusambaratika wka utawala wa Mugabe.

Wengi ni wanachama wa shirika ambalo limekuwa likiandaa maandamano mara kwa mara dhidi ya serikali ya Mugabe.

“Leo si kituo bali ni kikomo. Tunahitaji mabadiliko kamili,” alisema Chipo Parirenyatwa, mwenyekiti wa Shirika la Haki za Kibinadamu la Zimbabwe.

“Sifahamu ni vipi jeshi litaendesha mambo, lakini nina matumaini. Kuna haja ya kuwepo wka uchaguzi kwa njia ya amani na jamii ya kimataifa kushirikishwa.

LEAVE A REPLY