Raia wa Gambia waanza kuikimbia nchi yao

0
135

Maelfu ya raia wa Gambia wameripotiwa na shirika la BBC kuanza kuikimbia nchi hiyo kwa hofu ya kutokea vita.

Hatua hiyo inatokana na misimamo ya rais Yahya Jammeh na Adama Barrow ambao kila mmoja anataka atambuliwe kuwa rais wa nchi hiyo baada ya tarehe 19 mwezi huu.

Wananchi hao wanaodaiwa kukimbilia nchi ya jirani ya Senegal wanadaiwa kuieleza BBC kuwa hofu yao kubwa ni kutokea kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo hususani baada ya ECOWAS kuahidi kutumia jeshi la Senegal kumtoa madarakani Jammeh na huku jeshi la nchi hiyo likimuunga mkono rais Jammeh.

Mgogoro nchini Gambia ulianza baada ya rais Jammeh kuyapinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Adama Barrow na kudai uchaguzi huo ulikuwa na makosa mengi.

Wakati huo huo bado haijafahamika iwapo Adama Barrow aliyepo nchini Senegal ataapishwa nchini humo au atarejea Gambia kwaajili ya kula kiapo cha urais nchini mwake.

LEAVE A REPLY