Raia saba wa China wametakiwa kuondoka nchini kwa kukiuka sheria za uhamiaji

0
129

Raia saba wa China wametakiwa kuondoka nchini kutokana na kukiuka taratibu za ukazi, huku raia mmoja wa Uganda akishikiliwa kwa kuwa na hati 15 za kusafiria za Burundi na Madagascar kinyume cha Sheria.

Kamishna wa Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam, John Msumule amesema kuwa pia wanawashikilia raia wengine 25 wenye asili ya ki-Asia kwa kufanya kazi nchini kinyume cha sheria na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili wao pamoja na waajiri wao.

Pia Kamishna Msumule amesema wanawashikilia waajiri wawili kwa kosa la kuwatumikisha raia wa kingeni bila kibali na kuwataka waajiri kote nchini kuhakikisha wanafuata taratibu za uajiri kabla ya kuingiza raia wa kigeni kwani idara hiyo haitawafumbia macho.

Katika hatua nyingine Kamishna Msumule amesema wanapanga kuwataja hadharani maafisa wa idara hiyo ambao wamekuwa siyo waminifu wakishirikiana na wahamiaji haramu kughushi nyaraka za ukazi na vibali vya kazi kwa lengo la kuongeza uwajibikaji katika idara hiyo.

 

LEAVE A REPLY