R. Kelly ashambulia gerezani

0
30

Mwanamuziki wa R&B nchini Marekani, R Kelly ameshambuliwa na mahabusu mwenzake gerezani ambako anasubiri hukumu ya kesi yake.

 

Mwanasheria wa R Kelly, Steve Greenberg amesema kuwa R Kelly alishambuliwa katika gereza la Chicago Metropolitan Collection Center, ambako R Kelly anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake ya unyanyasaji wa kingono wa wanawake.

 

Mahabusu mwenzake na R Kelly, alimshambulia alipokuwa amekaa kwenye kitanda kwa kumpiga ngumi sababu ikiwa kusitishwa kwa kutembelewa gerezani kutokana na mashabiki wa R Kelly wanaoandamana nje ya gereza hilo.

 

R Kelly amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na kushindwa kupewa dhamana ambapo kesi yake hiyo, inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi huu Septemba.

LEAVE A REPLY