R. Kelly akumbwa na skendo nyingine ya unyanyasi wa kingono

0
173

Mwanamuziki nyota wa Marekani, R. Kelly amefunguliwa kesi ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamke aliyetajwa kwa jina la Faith Rodgers.

Katika mashtaka hayo, Faith  mwenye umri wa miaka 19 anadai kuwa alikutana na R. Kelly mwezi Machi mwaka jana na kwamba alimkatia tiketi ya ndege kumsafirisha kwenda jijini New York ili ahudhurie tamasha lake.

Amedai kuwa baada ya tamasha, mwimbaji huyo alimfuata chumbani kwake na kumlazimisha kufanya naye ngono huku akimnyanyasa kwa namna mbalimbali.

Kwa mujibu wa nyaraka za mashtaka hayo, R Kelly na Faith walikuwa wapenzi kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya hapo na kwamba alimuambukiza msichana huyo ugonjwa wa zinaa.

Alimtuhumu pia kwa kumfungia chumbani, studio na kwenye gari mara kadhaa kwa nia ya kumuadhibu kwa kushindwa kumtimizia haja zake za matamanio ya ngono.

Faith anadai kuwa R. Kelly alimuwekea mlinzi wa kike ambaye alikuwa anahakikisha haondoki kwenda mbali.

LEAVE A REPLY