R. Kelly akumbwa na kashfa ya kingono

0
102

Mwanamuziki wa Marekani, R. Kely amekuwa kwenye wakati mgumu baada ya filamu inayoelezea maisha yake kuanza kurushwa hewani huku ikionesha ukatili wa kingono aliokuwa akiwafanyia mabinti wadogo na baadhi ya wafanyakazi wa kike.

Filamu hiyo ambayo ni mtitiriko wa vipindi kadhaa imewashtua raia wa Marekani wakiwemo wasanii wenzake ambao walionesha kutofurahishwa nayo, na kutoa maoni yao ambayo huenda yakamuweka pabaya msanii huyo mwenye sauti ya kipekee duniani.

 

Miongoni mwa wasanii ambao wamezungumzia hilo ni John Legend ambaye alikubali pia kuonekana kwenye filamu, amesema anawaamini wanawawake hao na kwamba R. Kelly amewaumiza watu wengi kwenye maisha yao.

 

Neyo naye alifunguka ya moyoni na kuandika kwamba kitendo cha R. Kelly kufanya vitendo hivyo ni vitu ambavyo haviwezi kukubalika, kwani ni muhimu kuwalinda watoto zaidi kuliko kuulinda muziki.

 

Licha ya hayo, wasanii wakubwa kama Jay Z na Lady Gaga, wamekataa kuonekana kwenye filamu hiyo, ambayo inaaminika na wengi kuwa imetengenezwa ili kummaliza R.Kelly kimuziki.

LEAVE A REPLY