Quick Rocka akanusha kutoka kimapenzi na Kajala

0
224

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Quick Rocka amesema kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mugizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja.

Kauli hiyo ya Quick Racka zimekuja baada ya kuenea taarifa za wawili hao kuwa na mahusiano ya kimapenzi lakini mkali huyo amekanusha taarifa hizo.

Quick Rocka amesema hajawahi kutoka na mrembo huyo wa Bongo Movie ila n rafiki yake wa kawaida tu ila si mpenzi wake.

“Stori kuwa nilikuwa natoka na Kajala ilikuwa ya uongo, usitake nitafutia matatizo” alisema Quick Rocka.

Kwa sasa, imeonekana wawili hao hawana ukaribu kama ilivyokua zamani mpaka kupelekea kuwekana kwenye mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY