Queen Latifah kutunukiwa tuzo ya heshima kesho

0
182

Muigizaji maarufu nchini Marekani, Dana Owens ‘Queen Latifah’ anatarajia kutunukiwa tuzo ya heshima kwenye tamasha la The American Black Film Honors kesho.

Queen Latifah amesema amefarijishwa sana na heshima hiyo aliyopewa na inampa nguvu ya kuendelea kufanya anachokifanya kwenye Entertainment industry.

Msanii huyo ambaye anawania tuzo kubwa ya The Oscars Awards mwaka huu anatarajia kupokea tuzo ya Entertainment Icon Award kwenye sherehe hizo za American Black Film Festival zitakazofanyika jijini Los Angeles, Marekani.

Queen Latifah ameshawahi kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa za filamu nchini Marekani, The Emmy Awards na pia ameshawahi kushinda tuzo ya The Golden Globe.

Wasanii wengine wanaowania tuzo hizo ni pamoja na Terrence Howard maarufu kama Lucious Lyon kwenye series ya EMPIRE.

Tuzo za The American Black Film Festival Honors zitafanyika katika jiji la Los Angeles nchini Marekani kesho Ijumaa.

LEAVE A REPLY