Video: WAJUA: Team Kiba kuoa kwa Team WCB?

0
1052

Baada ya kauli ya staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba aliyoitoa mwaka jana kuwa ana mmiss staa wa lebo ya WCB, Mwajuma Abdul Juma a.k.a Queen Darleen ‘kuamshwa ilipolala’ tayari staa huyo wa kike nae ametoa la moyoni pia.

Kama utakumbuka walifanya pamoja ngoma ya WAJUA ambapo kila kiilichokuwa kikizungumzwa humo ni mapenzi tu na mahaba mazito.

Lakini sasa Queen Darleen ameweka wazi msimamo wake na ukweli ambao pengine ulikuwa ukifahamika kwa wafuatiliaji wachache wa nyanja ya burudani.

Queen Darleen amemkana Ali Kiba na kudai ukaribu uliokuwepo baina yao hata kabla hawajapata majina makubwa kwenye Bongo Fleva ni ‘ushkaji tu’ na si zaidi ya hapo.

Na Queen akaenda mbali zaidi kwa kudai wakati yuko karibu na Kiba (miaka hiyo) tayari alikuwa na mpenzi wake (Hamis Dakota) ambaye walifanikiwa kupata mtoto mmoja.

Queen anammiss Kiba? Ndio, nammiss kama mshkaji wangu na kama msanii mwenzangu ambaye tulifanya mengi kwaajili ya kufika hapa tulipo leo.

Queen ana ugomvi na Kiba? Hana, upinzani wa kikambi ni sehemu ya kukuza sanaa yao lakini yeye na Kiba hawana tofauti za aina yoyote.

Kiba akija kuomba ‘kuoa?’ hatukuwahi kuwa wapenzi na wala sio wapenzi kwa sasa. Ataanzia wapi?

LEAVE A REPLY