Queen Darleen akanusha kumtelekeza baba yao

0
120

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Queen Darleen ambaye ni dada wa Diamond amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wamemtelekeza baba yao.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni kuenea kwa habari katika mitandao ya kijamii kuwa mwanamuziki pamoja na kaka yake Diamond wamemtelekeza baba yao kwa kutompa msaada wa aina yoyote.

Katika mitandao ya kijamii zilisambaa video zikimuonyesha mzee huyo akilalamika huku akidai kwasasa ni mgonjwa na anahitaji msaada kutoka kwa watoto wake hao wawili.

Queen Darleen amedai kuwa picha ambazo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii ni za zamani hivyo sana hivyo watu wametunga histori ili kuwachafua.

Ameongeza kwa kusema kuwa baba yao wanampigia simu na kuongea nao kama kawaida ila kuwa watu wanataka kuwagombanisha na baba yao ila wao wapo vizuri na mzee wao na hakuna tatizo juu yao.

Habari zinasombaa katika mitandao ya kijamii kuwa Queen Darleen na Diamond hawataki kumsaidia baba yao bila sababu yoyote.

LEAVE A REPLY