Q Chilla ashangazwa na Harmonize

0
91

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Q Chief amefunguka na kusema kuwa mashabiki wengi wa muziki walijua atafanya kazi na Harmonize baada ya kufanya nyimbo kadhaa za pamoja.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja kufuatia mashabiki kuhoji ni kwanini wanamuziki hao hawajaachia wimbo wa pamoja kwa muda mrefu.

Q Chief ambaye alijizoelewa maarufu miaka kutokana na vibao vyake amesema kuwa kwasasa yeye ni msanii huru ambaye anaweza kufanya kazi na mtu yeyote ili muziki wake uende mbele.

Pia mwanamuziki huyo amedai yupo sawa na rais huyo wa Konde Gangs ingawa anashangaa yeye anasupport kazi Harmonize lakini Harmonize hapost za kwake.

Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa bifu ya Harmonize na Diamond halijamsaidia chochote hadi sasa licha ya kuwa upande wa Harmonize.

LEAVE A REPLY