Q Chilla afunguka wema aliofanyiwa na Jose Chameleone

0
35

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Q Chief, ameeleza kuhusu safari ya maisha yake kwenye muziki wakati alipokutana na msanii Jose Chameleone nchini Uganda ambapo alimpokea na kumuonyesha baadhi ya vitu walivyokuwa pamoja.

Q Chief amesema: “Nilipokuwa nchini Uganda msanii Jose Chameleone alinikaribisha vizuri na kunizungusha kila kona, hii ilitokana na heshima na upendo tuliokuwa nao.“

Pia amesema: “Ustahimilivu ndiyo unanijenga kuwa imara siku zote, nimekutana na watu sahihi kama Daxo Chali na Marco Chali ambao wamefanya mabadiliko kwenye muziki wangu.

Ameongeza kwa kseuma kuwa “Nafanyia kazi Albamu yangu mpya na tour yangu ambayo itakuja, kwa hiyo watu wajiandae kunipokea, mimi ni msanii ambaye napenda kuingia kwenye damu ya mtu na hiyo ndiyo maana ya mwanamuziki na muziki mzuri,” amesema Chilla.

Q Chief ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao mpaka sasa wana heshima zao kwenye muziki na bado wanafanya muziki.

LEAVE A REPLY