PSG yamsajili mtoto wa George Weah

0
176

Klabu ya Paris Saint-German imemsajili mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Liberia George Weah anayeitwa Tomothy Weah kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mshambuliaji huyo wa miaka 17 ametia saini mkataba wa miaka 3 na PSG klabu ambayo baba yake aliwahi kucheza kutoka mwaka 1992 hadi 1995.

Mnamo mwezi Septemba 2016, kinda Weah alifunga hat-trick katika ushindi wa 8-1 dhidi ya klabu ya Ludogorets katika mechi yake ya kwanza ya Uefa.

Baba yake mwenye umri wa miaka 50 kutoka Liberia aliwahi kushinda mara tatu taji la mwanasoka bora wa Afrika na mchezaji wa pekee wa Afrika kuwahi kushinda taji la Ballon d’Or mwaka 1995.

Alijipatia umaarufu katika klabu ya Monaco 1988 na kufanikiwa kuzichezea PSG na AC Milan muongo uliofuata.

Pia aliichezea Chelsea na Manchester City katika ligi ya Uingereza katika miaka ya mwisho ya soka yake.

Kuwasili kwa Keane haitakuwa mwisho wa Everton kutumia pesa nyingi chini ya meneja Koeman ambaye ana lengo la kuijaribu Swansea City iwapo watamuhifadhi kiungo wa kati mwenye miaka 27 kutoka Iceland Gylfi Sigurdsson.

The Toffees pia watafanya biashara na burnely katika msimu wa joto baada ya ripoti kwamba wameanza mazungumzo dhidi ya mshambuliaji Andre Gray.

LEAVE A REPLY