Profesa Jay arudi kwa kishindo kwenye game

0
26

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Profesa Jay amefunguka na kuthibitisha kuwa atatumia miaka mitano ambayo atakuwa nje ya Bunge kufanya muziki.

Profesa Jay amefunguka na kusema kuwa anataka kuhakikisha kuwa miaka hii mitano ni kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wa muziki wake kwa sababu moja ya vitu nilivyogundua ni kwamba bado wanamuhitaji.

Anaongeza kuwa hata wimbo mpya alioshirikishwa na Stamina ulitakiwa uwe umetengenezwa muda mrefu, lakini imewezekana mwaka huu kwa sababu yupo nje ya Bunge.

Pia amesema kuwa “Hata huu wimbo wa Stamina alinipigia simu kunielezea wazo muda mrefu sana, lakini kutokana na ratiba zangu kila siku nikawa namsubirisha. Lakini kwa sasa niko huru, ndiyo tukapata nafasi ya kufanya.”

Profesa anasema kwa sasa anakesha studio akitengeneza ngoma na pindi atakapokuwa tayari kuachia makombora atatoa taarifa.

LEAVE A REPLY