Profesa Jay ampongeza Diamond kufungua Wasafi Tv

0
302

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Professa Jay amempongeza mwanamuziki mwenzake, Diamond Platnumz baada ya kufungua kituo chake cha Radio na Tv nchini.

Profesa Jay ambaye ni mbunge wa Mikumi amesema kuwa jambo alilofanya Diamond ni jema sana kwa kila mpenda maendeleo na burudani nchini lazima atasapoti jambo hilo kwani linaleata maendeleo.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Profesa Jay ameandika ‘hili ni jambo jema sana ambalo kwa kila mpenda maendeleo na burudani  nchini ni lazima alifurahie,hongersa sana mdogo wangu @diamondpaltinumz  na timu yako nzima ya WCB #YAMETIMIA TUKO PAMOJA SANA.

Diamond amepokea pongezi nyingi sana kutoka kwa wasanii na watu mbalimbali kutokana na kufungua kituo hicho cha Tv ambacho kimeanza kurusha matangazo yake toka wiki hii kupitia king’amuzi cha Azam Chanel namba 122.

LEAVE A REPLY