Profesa Jay akanusha kumdisi Afande Sele kwenye nyimbo yake ‘Kibabe’

0
305

Mkali wa hip hop bongo, Prof Jay amekanusha kumdisi Afande Sele kwenye wimbo wake mpya wa ‘Kibabe’.

Profesa Jay ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia Chadema amedai kuwa mashairi hayo ni ya kawaida ambayo alimua kuyaweka.

Katika ngoma hiyo, kuna mstari usemao ‘Mwambieni mfalme wenu siti yangu aifute vumbi’, mstari ambao umekuwa ukizusha hisia kuwa ni dongo kwa Afande Sele ambaye amewahi kupata taji ya Mflame wa Rymes.

Profesa Jay amesema mstari huo ni wa kawaida na siyo dongo kwa mtu yeyote na wala hajawahi kuwa na tatizo na Afande Sele kwa hiyo ni vigumu sana kumsema kwa kutumia wimbo kwa kuwa ni mtu anayemuheshimu.

Kuhusu harakati za kisiasa, Jay amesema licha ya Afande Sele kuwa chama tofauti, si miongoni mwa wasanii waliojitokeza kumpinga wakati akigombea ubunge katika jimbo la Mikumi.

LEAVE A REPLY