Prof. Longinus Kyaruzi amrithi Dkt. Nyamajeje TCAA

0
171

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

Uteuzi wa Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara umekuja baada ya kumalizika kwa muda wa utendaji wa mtangulizi wake Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro.

Uteuzi: Rais Magufuli amemteua Prof. Kyaruzi kumrithi Dkt. Nyamajeje TCAA
Uteuzi: Rais Magufuli amemteua Prof. Kyaruzi kumrithi Dkt. Nyamajeje TCAA

Uteuzi wa Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara umeanza rasmi tarehe 16 Julai, 2016.

Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo Prof. Kyaruzi aliwahi kuwa mhadhiri wa uchumi kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam kisha kuwa naibu katibu mtendaji wa tume ya taifa ya mipango.

LEAVE A REPLY