Prof. Lipumba na Maalim Seif ‘uso kwa uso’

0
283

Bodi ya chama cha wananchi CUF, wanatarajia kuandaa utaratibu wa kuwakutanisha katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif na mwenyekiti wake, Prof.Ibrahim Lipumba ili kuwapatanisha kutokana na mgogoro ulioibuka na ambao unaendelea kukigawa chama hicho

Wajumbe wa bodi hiyo wamesema wanahuzunishwa na mgogoro ndani ya chama hicho mpaka kupelekea chama kukosa muelekeo kutokana na marumbano ya pande hizo mbili.

Mjumbe wa bodi CUF,Peter Malebo ameeleza kuwa watawaita viongozi hao makao makuu ili waweze kupata suluhu na kumaliza mgogoo huo unao endelea.

Hivi karibuni, baraza la uongozi la chama cha Wananchi (CUF), lilitangaza kumfukuza uanachama Lipumba.

Amefukuzwa kwa kile kilichoelezwa kuwa amekwenda kinyume na katiba ya chama na kufanya uasi kwa wanachama.

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kwenye taarifa yake amesema kuwa ofisi yake inamtambua kuwa Prof. Lipumba ni mwenyekiti halali ya wa chama cha wananchini CUF .

Kutokana na kauli hiyo ya msajili wa vyama vya siasa ikaibua mgogoro zaidi ndani ya chama hicho mpaka kupelekea kutoelewana katika ya Prof. Lipumba na katibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamad.

LEAVE A REPLY