Producer amtetea Zuchu kashfa ya kucopy wimbo wa Cheche

0
48

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, Mocco Genious amefunguka kuhusu wimbo wa Zuchu ‘Cheche’ kufutwa YouTube baada ya taarifa kusikika kuwa nyimbo hiyo wame Copy.

 

Mocco ameeleza kwa undani huku wengine wakidai kuwa Producer ndio ilikuwa sababu ya ngoma hiyo kufutwa kwani ali sample beat ya mtu mwingine.

 

Mocco amemtetea Zuchu kutokana na mistari aliyoimba kwenye ngoma hiyo kwa kudaiwa kuchukua mistari kwenye baadhi ya ngoma ya mtu mwingine.

 

Pa amesema kuwa Zuchu alikuwa anaenda Studio kurekodi na wimbo mzima umerekodiwa Studio kwahiyo alikuwa anaona kabisa Zuchu anavyoandika wimbo mwanzo hadi mwisho.

 

Wimbo wa Cheche wa Zuchu aliomshirikisha Diamond Platnumz ulifutwa kwenye mtandao wa Youtube lakini baadae ukarudishwa kwenye mtandao huo.

LEAVE A REPLY