Prezzo awachimba mkwara wanaume wanaomfatilia mpenzi wake

0
151

Mwanamuziki mkongwe kutoka Kenya, Jackson Makini maarufu kama CMB Prezzo licha ya kuachana na mpenzi wake lakini amewachimba mkwara wanaume wa nchini humo wanaomfuatilia mpenzi wake huyo Michelle Yola.

Prezzo amedai kuwa japokuwa ameachana na mpenzi huyo lakini bado wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kuyaweka mambo sawa ili warudiane.

Kutoka na mazungumzo yanayondelea kati ya wawili hao hivyo Prezzo amewaonya wanamume  waanaojaribu kumshawishi mrembo huyo waweze kuwa kwenye uhusiano.

Mkali huyo amesema kuwa endapo mtu yoyote atakuwa nae kwenye mahusiano atahakikisha anapambana naye.

Ameendelea kusema “Ni kweli nipo kwenye mgogoro na Michelle katika uhusiano wetu, bado sijatangaza kama tumeachana, japokuwa kuna habari kwenye mitandao zinadai tumeachana.

Pia amesema “Mazungumzo yanaendelea kwa ajili ya kuweka sawa mgogoro wetu, hivyo sipo tayari kuona mwanamume mwingine akijipeleka kutaka kuanzisha uhusiano na Michelle.

LEAVE A REPLY