Pretty Kind kuandika barua ya msamaha kwa Naibu waziri Shonza

0
245

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Pretty Kind aliyefungukiwa kutojihusisha na muziki kwa miezi sita amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuandika barua kwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Mihezo, Juliana Shonza kwa ajili ya kuomba msamaha.

Pretty Kind amesema kuwa ameamua kuandika barua ya msamaha kwasababu amekuwa na wakati mgumu baada ya kufungiwa asijihusishe na muziki kwa miezi sita.

Mwanamuziki huyo pia amesema kuwa ataandika barua hiyo hata apunguziwe adhabu kwani adhabu aliyopewa ni kubwa sana.

Pia amesema kuwa ‘Nimeshaomba sana msamaha na ninaendelea kuomba ambapo kwa sasa ninaandika barua ya kuomba msamaha kwa naibu waziri maana maisha hayaendi’.

Mwanamuziki huyo alifungiwa na Naibu waziri, Juliana Shonza kutokana na kuweka picha za utupu katika mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY