Post ya mti wa Krismasi yamtokea puani Ronald Koeman wa Everton

0
215

Mashabiki wa timu ya Everton wamempa ‘makavu live’ kocha wao Ronald Koeman baada ya kuonyesha mti wa Krismasi alioupamba nyumbani kwake ukiwa umejaa rangi nyekundu ambazo zinatumiwa na wapinzani wao wa jadi Liverpool.

Mashabiki hao ambao hata hivyo huenda wametafsiri rangi hizo kama kocha wao kuisapoti klabu ya Manchester United ambayo pia inatumia jezi nyekundu huku vigogo hao wa jiji la Liverpool wakiwakaribisha mashetani wekundu kwenye dimba la Goodson Park siku ya Jumapili.

Ronald Koeman ameomba msamaha kwa mashabiki wake na kudai mti huo umepambwa hivyo na mke wake ambaye hana uzoefu wa mahaba ya mashabiki kwa timu zao kuwa mahaba hayo huenda mbali kuliko alivyotarajia.

Mashabiki wa Everton walionyesha mti mbada ambao walitarajia kocha wao aupambe nyumbani kwake.

Post ya mti wa Krismasi uliotaka kumponza Koeman

koeman-mistake

Zawadi ya mti alioambiwa Koeman aupambe kwake

screen-shot-2016-12-02-at-19-04-22

LEAVE A REPLY