Pongezi za Wema Sepetu kwa RC Makonda

0
154

Mugizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na utendaji kazi wake.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Wema amepost picha ya mkuu huyo na kuandika ujumbe unaowataka wakazi wa Dar es salaam kujivunia mkuu huyo kutokana na utendaji wake wa kazi.

Ameanza kwa kuandika “Tanzania Kwanza. Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi… Mungu akakutangulie katika kazi zako za lengo la kuijenga Tanzania yako izidi kuwa zaidi ya ilipo sasa,”.

Pia ameongeza kwa kuandika, “Ipo siku wataelewa tu, The Man Himself… Call Him Mr Dar-es-salaam… Viva RC wangu…. Viva Rais wangu…. #UzalendoKwanza … cc @paulmakonda May everything you wish well for your Nation Be…. We support you fully,”

Wema Sepetu toka arejee CCM kutoka Chadema amekuwa karibu na mkuu wa mkoa huyo licha ya kumtaja kwenye orodha ya wasanii wanaotumia dawa za kulevya.

LEAVE A REPLY