Polisi nane wameuawa na watu wasiojulikana wilayani Rufiji

0
289

Polisi saba waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, wanadaiwa kuuawa usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, lakini akasema taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani.

Miili ya askari saba waliouawa na majambazi wilayani Rufiji mkoani Pwani jana.
Miili ya askari saba waliouawa na majambazi wilayani Rufiji mkoani Pwani jana.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.

Imeelezwa kwamba majambazo hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.

LEAVE A REPLY