Polisi 14 watimuliwa kazi Nigeria kwa kuwauzia wahalifu silaha na kushirikiana nao

0
129

Jeshi la Polisi nchini Nigeria limewafuta kazi maafisa wake 14 kwa tuhuma za kushiriki kwenye uhalifu unaotendeka nchini humo kwa kuwauzia silaha wapiganaji na wahalifu mbalimbali wakiwemo watekaji nyara.

Gazeti la nchi hiyo, Punch limeripoti kuwa maafisa hao wanadaiwa kuuza silaha za moto ikiwemo binduki, risasi, mabomu na milipuko mingine jambo linalochangia kuota mizizi kwa genge la wahalifu na wimbi la uhalifu nchini humo.

Gazeti la Punch limedai kuwa maafisa tisa kati ya hao 14 waliwekwa hadharani mbele ya waandishi wa habari katika jiji la Abuja.

Maafisa hao wa polisi pia wanatuhumiwa kushirikiana na wezi wa mifugo kuiba ng’ombe na kufanya ujambazi kwenye maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Baadhi ya silaha ikiwemo Bunduki zilikamatwa kwenye upekuzi wa watuhumiwa hao.

Picha: Punch Newspaper

LEAVE A REPLY