Polepole: CCM kwasasa ina misingi ambayo inawabana viongozi wasiotosheka

0
83

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho kwasasa kimeweka misingi ambayo inawabana viongozi wasiotosheka.

Polepole amesema kuwa Chama chao kinalinda misingi na Itikadi zake ambazo ni kuheshimu utu wa mtu pamoja na kuwatumikia raia hivyo kwa kiongozi ambaye hawezi kufanya hayo lazima atakimbia.

Pia Polepole amesema kuwa mwanachama anayehama chama chetu kwasababu sio misingi na Itikadi zetu.

Vile vile ameongeza kuwa ni dhambi kubwa kumhukumu mtu anapohama chama kimoja kwenda kingine.

Polepole amesisitiza kuwa CCM kwasasa imeweka misingi migumu itakayowabana wasiotosheka na wasio na kiasi ndio maana tumeamua kuweka sheria ya mtu mmoja, cheo kimoja. Sheria ambayo itawabana wenye kutaka vyeo vingi kwa wakati mmoja.

LEAVE A REPLY