Picha ya Diamond na dada yake yazua gumzo

0
279

Baadhi ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva walishikwa na butwaa baada ya kusambaa picha za party ya Diamond Platnumz zikimuonesha akiwa na dada yake Esma katika mazingira ya kutatanisha kutokana na kujiachia kwao.

Jumapili iliyopita mwanamuziki huyo alifanya party ya birthday yake katika boti kwenye kisiwa cha Mbudya kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo kwenye party baadhi ya watu walihudhuria kwa mihariko maalum.

Katika sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya boti katika Bahari ya Hindi, Dar, ilihudhuriwa na watu wa karibu yaani wanafamilia na marafiki wachache wa Diamond.

Diamond na dada yake walipiga picha wakiwa kwenye pozi huku wakiwa wameshikilia glasi za vinywaji ambapo Mbongo-Fleva huyo alikuwa kifua wazi huku Esma akiwa mapaja wazi.

Waliohudhuria katika sherehe hiyo na wale walioiona katika mitandao ya kijamii walipigwa na butwaa huku wakieleza kwani zaidi huwa linakaliwa na watu ambao ni wapenzi.

Diamond alikuwa akisherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Oktoba 2, mwaka huu ambapo iliendelea mpaka Oktoba 7, mwaka huu ambayo ilikuwa ndiyo hitimisho.

 

LEAVE A REPLY