Papii Kocha kurudi FM Academia

0
67

Mwanamuziki wa Dansi nchini Johnson Nguza Viking ‘Papii Kocha’ amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kurudi katika bendi yake ya Ngwasuma.

Papii Kocha ametangaza kujiunga na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ aliyokuwa akiitumikia kabla ya kupatwa na majanga ya kifungo cha maisha na baadaye kupata msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Papii Kocha amesema kuwa hafikirii kujiunga na bendi nyingine yoyote zaidi ya kurudi kwenye bendi yake hiyo ya zamani kwani bado anaipenda.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kwasasa anafanya kazi ya muziki kwenye maonesho mbalimbali akiwa na baba yake (Babu Seya) kama wasanii binafsi.

Msanii huyo anataka kujiunga na FM Academia ambapo alikuwa anafanyia kazi kabla ya kufungwa kifungo cha maisha jela.

LEAVE A REPLY