Papii Kocha awashukuru mashabiki waliojitokeza kwenye show yake

0
63

Mwanamuziki wa dansi nchini, Papii Kocha amewashukuru mashabiki pamoja na baadhi ya wasanii waliojitokeza kwenye show yake iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam.

Papii Kocha amesema kuwa amefurahishwa sana na watu wote walioitokeza kwenye show yake kwani wameonesha jinsi gani wanamkubali na walimmisi wakati alipkuwa gerezani kabla ya kutoka kwa msamaha wa rais.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa show yake hiyo ni mwanzo tu na anategemea kufanya show nyingi ili kurudisha hadhi ya muziki wa dansi ulioonekana kama kupoteza ladha kwa mashabiki wa muziki huo.

Pia Papii Kocha amewashakuru waandaji wa show kutokana na maandilizi waliyofanya kwenye show hiyo iliyobamba mwishoni mwa wiki.

Papii Kocha na baba yake mzazi, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya juzi walifanya show kubwa kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela walipokuwa wanatumikia kifungo cha maisha.

LEAVE A REPLY