Papii Kocha ashangazwa na Koffi Olomide kwenye wimbo wa Waah

0
24

Mwanamuziki wa dansi nchini, Papii Kocha amesema amemshangaa mkongwe wa dansi kutoka Congo DR, Koffie Olomide katika wimbo wa Waah alioshirikiana na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platniumz kwa kuimba kama rapa.

 

Papii Kocha amesema amemshangaa Koffie kuimba katika ngoma hiyo kama rapa badala ya muimbaji.

 

Pia Papii amesema kuwa “Mimi nilichomshangaa nnavyomjua Koffi yeye ni muimbaji na siyo rapa lakini katika wimbo huo amefanya kurap.

 

Ameongeza kwa kusema kuwa “Jambo lingine lililonishangaza mimi nilivyosikia wametoa wimbo mpya nilijua kutakuwa na jipya lakini badala yake kumbe ilikuwa ni kuingizia vipande vya wimbo wa Papaa Mobimba na kuufanya wimbo huo uonekane kama remix ya wimbo huo,”.

 

Wimbo huo kwasasa una jumla ya watazamaji milioni mia mbili na hamsini toka ulipoachiwa mwishoni mwa mwaka wa jana.

LEAVE A REPLY