Papii Kocha afunguka anachokipenda

0
317

Mwanamuziki wa dansi nchini, Papii Kocha ameeleza starehe ambayo anaipenda baada ya kuachiwa huru.

Papii Kocha amefunguka hayo wakati anafanya mazoezi ya kujianda na tamasha la Rhumba ambalo litafanyika siku ya Ijumaa ikiwashirikisha wasanii kama Barnaba, Ruby na kundi la  Sauti Sol kutoka nchini Kenya.

Papii Kocha ameeleza vitu ambavyo alikuwa anavikumbuka wakati akiwa jela, ambapo amesema, “nilikuwa nau-miss muziki napenda sana muziki, nilikuwa napata nafasi ya kuimba lakini nikiwa huku inapendeza zaidi, mimi sio mtu wa wanawake na sifagilii hizo drama nina mke wangu inatosha na starehe yangu kubwa ni kuimba”

Aidha Papii Kocha amesema yeye sio mlevi na wala hatumii vinywaji, kwa sababu alishatumia na sasa inatosha.

Pia amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumrudisha uraini na kusema anampenda na anamuomba Mungu ampe maisha marefu yeye pamoja na familia yake.

Pia Papii Kocha amesema amjipanga vya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri kwenye onesho la burudani.

Tamasha la Rhumba Night linalotarajiwa kufanyika, Ijumaa ambapo wasanii wakubwa kutoka Kenya, akiwemo kutoka kundi la Sauti Soul wanatarajiwa kutumbuiza.

LEAVE A REPLY