P. Diddy atarajia kupata mtoto mwingine

0
115

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, P Diddy anatarajia kuitwa baba kutoka kwa mchumba wake, Cassie ambaye anaujauzito.

Katika picha mbalimbali zilizosambaa juzikati, zilikuwa zikimuonesha Cassie akiongozana na P Diddy huku tumbo lake likimuonesha kuwa ni mtu mwenye ujauzito.

Endapo Cassie atajifungua salama, atakuwa mtoto wake wa kwanza kuzaa na rapa huyo ambaye kwa sasa ana watoto sita aliozaa na wanawake tofauti.

Katika mahojiano aliyowahi kufanya hivi karibuni, P Diddy alikaririwa akisema; “Nawapenda watoto wangu, naelekea watoto nane sasa bila kuwa na tatizo.”

LEAVE A REPLY