Oxfam yazilaumu nchi tajiri kuhusu wakimbizi

0
177

Shirika la kusaidia wakimbizi la OXFAM International, limezitupia lawama nchi sita tajiri zaidi duniani za Marekani, China, Japan, Ujerumani na Uingereza kwa kuwahifadhi wakimbizi wachache zaidi duniani ikilingwanishwa na uwezo wao.

Nchi hizo sita zinakadiriwa kuhifadhi wakimbizi milioni 2.1 sawa na asalimia 8.88 ya wakimbizi wote duniani huku nchi maskini zaidi zikikubali kuwahifadhi wakimbizi wengi zaidi hivyo kuzidi kuongeza umaskini kwenye mataifa hayo.

Nchi za Jordani, Uturuki, Pakistan, Lebanon, Afrika Kusini na sehemu ya Palestina ambayo imevamiwa na kukaliwa kimabavu zinahifadhi wakimbizi zaidi ya asilimia 50.

Ingawa nchi ya Ujerumani hivi karibuni ilitoa nafasi ya kuongeza nafasi za kupokea wakimbizi, bado mataifa mengine yamebaki kimya na tofauti ya uhifadhi wa wakimbizi baina ya nchi tajiri na nchi maskini umebaki kuwa mkubwa sana.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Oxfam, Winnie Byanyima amedai kuwa ni aibu kubwa kwa mataifa mengi kugeuza migongo yao dhidi ya watu ambao wamekimbia kwao na aambao mara nyingi wanapitia hatari nyingi ili kupata usalama.

Inakadiriwa kuwa hadi sasa kuna wakimbizi zaidi ya milioni 65 duniani kote waliokimbia nchi zao kutokana na mauaji, fujo na machafuko.

LEAVE A REPLY