Ommy Dimpoz: Ukiwa staa lazima ujitambue

0
308

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amezumgumzia suala lake la kusafiri mara kwa mara na kudai kuwa huwa haendi kula bata pekee bali ni kutafuta ‘connection’.

Ommy Dimpoz amefunguka hayo baada ya kuulizwa safari zake za kwenda kula bata nchi za nje, pamoja na kupiga picha na wasanii wakubwa wa mataifa mengine.

Dimpoz amefunguka na kusema kuwa “Sijaelewa watu wakisema bata wanaamanisha nini ni kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa sisi ni ‘brands’, watu wenye ushawishi nikikufungulia email yangu nitakuonesha mialiko, mingine hadi naikataa ili mienendo yangu iendane na kazi, pia connection zinapatikana na tunazitumia vizuri”.

Pia amesema kuwa  “Kitu akifanya Ommy kinageuka kuwa bata kwa mfano juzi tu nimetoka kuchukua tuzo za Afrimma, lakini watu hawajauliza hilo, ukishakuwa brands na ukijitambua mambo mengine yanakuwa ni rahisi sana”.

Pia Ommy Dimpoz amesema kuwa tayari ameshafanya kazi tatu na wasanii wakubwa wa kimataifa na mwisho wa mwezi huu ataenda ku-shoot nao video.

LEAVE A REPLY