Ommy Dimpoz atoa milioni moja kuchangia Kisarawe

0
36

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ameahidi kuchangia milioni moja katika harambee ya Tokomeza Zero ilioandaliwa na Jokate Mwegelo wa Kisarawe.

Katika kampeni ya Tokomeza Zero iliandaliwa na DC wa Kisarawe Joketi Mwegelo iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbali mbali wa Serikali walihudhuria kwenye hafla hiyo lakini pia pamoja na wadau mbalimbali wa Sanaa ikiwemo wasanii.

Katika hafla hiyo walifanikiwa kuongea viongozi mbalimbali na wadau mbalimbali katika kutoa ahadi ya kuchangia angalau chochote walichojaliwa nacho kwa ajili ya kupata pesa zitakazo saidia kujenga shule ya kwanza ya bweni ya wasichana katika wilaya hiyo ya kisarawe.

Ommy Dimpoz alikuwa kama Suprise kwa watu hawakujua kama yupo na alipotokea lifanikiwa kufanya show yake ya kwanza Tanzania baada ya kutoka kuumwa na pia alihidi kutoa au kuchangia Tsh milioni moja kwa ajili ya kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe.

LEAVE A REPLY