Ommy Dimpoz ataja nyimbo anazozikubali kutoka WCB

0
794

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema kuwa nyimbo anazozikubali kutoka kwa wasanii wa WCB ni ‘Kwa Ngwaru’ ya Harmonize na ‘Pochi Nene’ ya Rayvanny.

Ommy Dimpoz amesema kuwa anazikubali sana nyimbo hizo kutokana na ubora pamoja na ubunifu wa wasanii hao kwenye ngoma hizo.

Kwa Ngwaru ni ngoma mpya ya Harmonize aliyomshirikisha Diamond Platnumz ambayo inaendelea kufanya vizuri hadi sasa.

Pia Ommy ameitaja ngoma ‘Pochi Nene’ ambayo imeimbwa na Rayvanny akimshirikisha producer S2kizzy ambayo nayo inafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio na Tv nchini.

Ameendelea kusema nyimbo nyingi za WCB ni kali ila kwa upande wake amezipendekeza hizo ambazo kwasasa zinafanya vizuri.

Ommy Dimpoz kwasasa anatamba na wimbo wake ‘Wanje’ aliomshirikisha mwanamuziki kutokea nchini Nigeria.

LEAVE A REPLY