Ommy Dimpoz apata mwaliko NBA

0
132

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ni miongoni mwa mastaa watatu wa Afrika ambao wamepewa mwaliko rasmi wa kuhudhuria michezo ya NBA All-Star nchini Marekani.

Michezo hiyo ya NBA All-Star itafanyika mjini Chicago nchini Marekani kuanzia February 14 hadi 16 mwaka huu.

Dimpoz ambaye ameutaja mwaliko huu kama bora na mkubwa kwa mwaka huu, ataungana na Sho Madjozi wa Afrika Kusini na Jidenna wa Nigeria & Marekani.

Mwaliko huu ni kutoka Chama cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani – NBA, kupitia NBA Africa ambao wamemgharamia kila kitu ikiwemo Usafiri wa ndege kwenda Marekani.

Gharama hizo pia utahusisha usafiri wa ndani na gharama za kuishi akiwa pamoja na meneja wake Seven Mosha katika tukio hilo kubwa la mwaka nchini Marekani.

LEAVE A REPLY