Ommy Dimpoz aonekana nchini Kenya

0
122

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ameonekana nchini Kenya baada ya kipindi kirefu ambacho hakuonekana kutokana na kuugua.

Ommy Dimpoz amekuwa kimya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii toka Decemba Mosi mwaka jana. Kuliibuka taarifa za yeye kuzidiwa na kupelekwa nchini Ujerumani kwaajili ya matibabu  tena lakini taarifa hizo zilitupiliwa mbali na watu wake wa karibu.

Baada ya kimya kirefu Ommy Dimpoz ameonekana nchini Kenya akiwa na msanii wa Kenya anayejulikana Kama Willy Paul Msafi.

Willy Paul ameposti picha inayomuonyesha akiwa na Ommy Dimpoz katika ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza kwa maneno yaliyosomeka “Happy to see my Brother”.

Ommy Dimpoz na Willy Paul wamekutana Kenya, bado haijajulikana iwapo wawili hao wamekutana kwa lengo la kudumisha urafiki au ni kazi pekee.

LEAVE A REPLY