Ommy Dimpoz afungukia msaada wa Gavana Joho

0
109

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amefunguka na kusema kuwa Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ndiye mtu ambaye alimsaidia kwenye swala la matibabu kuanzia mwanzo anaumwa mpaka anakuja kupona.

Ommy Dimpoz amezungumza na Redio Milele ya nchini Kenya na kusema kuwa alikutana na Joho siku ya ndoa ya Alikiba ambapo wakati wa chakula alikabwa na chakula basi ndio mwazo wa kuzungumza swala la matibabu lilianzia hapo

Ommy Dimpoz amesema “Labda kitu nitakachoweza kusema ni Sultan anasupport kila mtu umenielewa, watu wengi anawasupport na naweza kusema kama mimi kipindi chote nimeumwa pia ameweza kuniuguza na nimekuwa chini ya uangalizi wake kwa kipindi hicho chote.

Kwa sababu nataka nikwambie wakati naanza kuumwa nimepata ile siku nimepata tatizo lile ghafla, tulikuwa kwenye harusi ya Kiba, tukiwa tunakula na yeye alikuwepo pale.

So nikawa ghafla kama nimekabwa hivi watu wote wakashtuka hivi na hivi ndio story ya hospitali pale ikaanza. So mtu kama ana uwezo kwanini akuwachie njiani wakati tayari alishakuanzisha kwenye matibabu,”.

LEAVE A REPLY