Ommy Dimpoz afunguka mahusiano yake na mastaa Bongo

0
251

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi na mwanamke yeyote maarufu nchini.

Ommy amesema kuwa matukio yote ambayo yalikuwa yanatokea kipindi cha nyuma yalikuwa hayana ukweli wowote.

Mwanamuziki huyo amedai kuwa hajawahi kutoka kimapenzi na wanawake yeyote maarufu wa kibongo na hata stori za kutoka kimapenzi na Wema Sepetu haikuwa kweli.

Ommy amesema wabongo wengi hawatumii akili kwani wanashindwa kutofautisha jina la Ommy Dimpoz na Omary kwani safari zote anazofanya nje ya nchi huwa anaenda kikazi.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo unaokwenda kwa jina la Yanje aliomshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria.

LEAVE A REPLY