Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amefunguka na kusema kuwa kutokana na kwamba marafiki zake wa karibu kuwa na familia na yeye anatarajia kuwa na familia.
Â
Ommy amesema kutokana na kwamba marafiki zake karibu wote wana familia yeye anapambana kupata mwanamke ambaye anauwezo wa kumtunza kutokana na afya yake.
Â
Anasema anahitaji mwanamke anayejua kupika uji supu na hata kumjali mgonjwa kwa kila hali kutokana na kwamba yeye siyo mzima sana.
Â
Akizungumzia mahusiano yake ya kikazi yeye pamoja na Meneja wake Seven Mosha, Ommy anasema hajawahi kugombana na menneja wake kwa kuwa amekuwa familia yake.
Â
Ommy amesema yeye atabaki nyumbani kwa kuwa alisha ahidi. “Mimi sitakwenda nje, Mimi ni wenu tuu…Haijalishi ni mkoa gani lakini mimi nitaoa nyumbani”.
Â
Wimbo mpya ya Dimpoz imekuja mwezi mmoja baada ya kutoa wimbo wa ‘Ni wewe’ alioutoa kwa ajili ya kumtukuza Mungu kutokana na kumponya ugonjwa uliomuweka kitandani kwa muda mrefu.