Ommy Dimpoz achukulia poa maneno ya Steve Nyerere

0
125

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema alichukulia poa maneno ya Steve Nyerere aliyoyasema kwamba hataweza kuimba tena kutokana na ugonjwa alioupata.

Ommy amesema kwamba kipindi chote alichokuwa akiugua amefundishwa mengi na ugonjwa wake na kugundua kwamba duniani ni sehemu ya kupita tu hivyo hakuna sababu yeyote ya watu kuchukiana au kununiana kwa sababu maisha ni mafupi na hakuna anayeijua kesho yake.

Amesema “Naweza kusema kwamba zamani nilikuwa na bifu sana yani ni ile kusema hivi nikanyage bahati mbaya nikukanyange makusudi ila kwa sasa nimeona ni vyema kuchukulia kila kitu poa ili maisha yaendelee.

 Pia ameendelea kusema kuwa ‘sihitaji tena mijadala ndo maana unaona hata mambo yangu na Steve yalikuja kuwa kama utani. Maisha yanabadilika hivyo tunapaswa kujifunza jambo ili tuweze kwenda sawa na maisha”.

Lakini pia Ommy amewataka watu, pamoja na wasanii wasiwe wanafiki katika maisha ya kila siku na hii ni baada ya mkuu wa mkoa kuposti kuwa watu wampe ushirikiano kwa wimbo wake kama walivyomposti akiwa ugonjwa na sio kumsapoti kinafiki ili kuondoa lawama.

LEAVE A REPLY